Berlin. Ujerumani yaporomoka kielimu.
13 Septemba 2006Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo katika bara la Ulaya, OECD, mfumo wa elimu wa Ujerumani umeporomoka nyuma ya mataifa mengine yenye viwanda.
Uchunguzi wa suala la elimu wa OECD unaonyesha kuwa Ujerumani haitoi wahitimu wa kutosha wa vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu kuweza kutumika katika mahitaji yanayozidi katika soko la kazi la kimataifa. Ripoti hiyo pia inashauri kuwa watoto kutoka mataifa yanayoendelea huenda wakawa katika nafasi nzuri kwa mahitaji ya karne ya 21 kuliko watoto wa mataifa ya Ulaya na Marekani kwasababu wanasemekana kuwa wanaweza kujibadilisha haraka kutokana na mazingira yanavyohitaji.