BERLIN : Ujerumani yaongeza muda wa wanajeshi wake Sudan
22 Septemba 2005Serikali ya Ujerumani imekubali kwamba wanajeshi wake wataendelea kubakia angalu kwa miezi sita katika shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kusini mwa Sudan ili mradi bunge litowe idhini yake.
Mamlaka hayo yanawarauhusu wanajeshi 75 wasiobeba silaha wengi wao wakiwa ni waangalizi wa kijeshi kusimamia makubaliano ya amani yaliofikiwa kati ya serikali na waasi wa kusini mwa Sudan hapo mwezi wa Februari.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck amesema ni wanajeshi saba tu wa Ujerumani ambao hadi hivi sasa wako nchini Sudan kwenyewe kutokana na matatizo ya kupta viza lakini anatumai wanajeshi wengine 50 watakuwako nchini humo kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Ni wanajeshi 2,100 tu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa tayari wako nchini Sudan hivi sasa kati ya wanajesdhi 10,000 waliopangwa kuwekwa nchini humo.