BERLIN: Ujerumani yajitolea kuongoza jeshi la wanamaji
27 Agosti 2006Matangazo
Ujerumani ipo tayari kubeba jukumu la kuongoza majeshi ya wanamaji kuambatana na mpango wa Umoja wa Mataifa kupeleka vikosi nchini Lebanon.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amesema, Ujerumani imejitolea kuongoza vikosi vitakavyolinda pwani ya Lebanon.Kwa mujibu wa jarida la Der Spiegel,serikali ya Ujerumani inatazamia kuchangia wanajeshi 1,200 katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachotazamiwa kwenda Lebanon.Lakini,wizara ya ulinzi haikusema cho chote kuhusu ripoti hiyo.