Berlin: Ujerumani yaitisha amani na ushirikiano
13 Novemba 2003Matangazo
Waziri wa mabo ya nje wa Ujerumani Joschka Fischer aliitisha ufumbuzi wa amani kuhusu mzozo wa kisiasa wa Georgia hiyo jana, katika mazungumzo pamoja na waziri mwenzake wa Georgia mjini Berlin. Duru za ujumbe wa Georgia zilisema Fischer alimwambia Irkali Menagarishvili katika mkutano wao, kwamba Berlin inachunguza kwa makini hali ya mambo. Rais Eduard Shevardnadze wa Georgia anapambana na viongozi wa upinzani wanayemtaka ajiuzulu, baada ya uchaguzi wa bunge tarehe pili Novemba, ambao wanasema ulifanyiwa ulaghai. Hiyo jana Fischer alionana pia na waziri wa mambo ya nje wa Armenia Vartan Oskanian na Vilajat Gulijev wa Azabeijan, kujadili masuala ya kimkoa na kimataifa, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, ambayo haikutoa maelezo zaidi.