BERLIN: Ujerumani yaiadhibu Sweden
17 Agosti 2006Matangazo
Katika mechi yake ya kwanza tangu kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya kuwania kombe la dunia, timu ya Ujerumani iliicharaza Sweden mabao 3:0 katika mchuano wa kirafiki jana usiku.
Mechi hiyo iliyochezwa mjini Gelsenkirchen hapa Ujerumani, ilikuwa ya kwanza ya kocha mpya wa Ujerumani, Joachim Löw, aliyechukua nafasi ya kocha aliyeondoka, Jürgen Klinsmann.