Berlin. Ujerumani yaahidi kuongeza msaada.
28 Oktoba 2005Serikali ya Ujerumani imesema kuwa itaongeza mchango wake wa kifedha katika juhudi za kupeleka misaada katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi nchini Pakistan.
Msemaji wa serikali amesema kuwa Ujerumani itaongeza Euro milioni tano katika Euro milioni 20 ilizokwisha ahidi.
Fedha hizo zitatumika kimsingi katika kuwapatia chakula wahanga kwa maelfu walionusurika na tetemeko hilo.
Baadhi ya fedha hizo pia zitakwenda katika juhudi za ujenzi mpya katika eneo hilo.
Katika mkutano wa umoja wa mataifa wa wafadhili siku ya Jumatano, zaidi ya nchi 60 zimeahidi kiasi cha Euro milioni 430 za misaada kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Pakistan.