BERLIN : Ujerumani yaadhimisha miaka 15 ya muungano
3 Oktoba 2005Ujerumani leo yaadhimisha miaka 15 ya umoja wa taifa ikiwa chini ya mashaka ya kisiasa yaliochochewa na matokeo tata ya uchaguzi wake mkuu na mzozano mkali juu ya nani anayepaswa kuwa kiongozi mpya wa nchi.
Uchaguzi huo wa taifa ambao ulikuwa haukukamilika umemalizika hapo jana wiki mbili kuliko iliyokuwa imepangwa kwa uchaguzi wa mji wa Dresden uliuoko mashariki ya Ujerumani ambapo umeimarisha nafasi ya uongozi kwa kiti kimoja kwa kiongozi wa kihafidhina Angela Merkel ambaye ana wingi wa viti vitatu zaidi katika bunge la taifa.Uchaguzi huo wa Dresden uliahirishwa kutokana na kifo cha mgombea.
Ingawa matokeo yake hayawezi kubadilisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa Septemba 18 ambayo hayakutowa mshindi dhahiri kati ya vyama vikuu vya kisiasa kile kinachotawala cha SPD cha Kansela Gerhard Schroeder na cha kihafidhina CDU matokeo hayo yanaweza kuimarisha madai ya Merkel kiongozi wa CDU kuwa Kansela mpya wa Ujerumani.
Ujerumani inaadhimisha siku hii ya leo ya kuungana kwa Ujerumani mbili miaka 15 iliopita ambayo ni siku ya mapumziko kwa shamra shamra nchini kote na sherehe rasmi zinafanyika katika mji wa mashariki wa Potsdam kwa kumjumuisha Rais Hörst Koehler na kiongozi wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl na iliokuwa Urusi Mikhail Gorbachov.