BERLIN : Ujerumani kuungoza tena kikosi maalum
23 Agosti 2006Matangazo
Ujerumani imerudia tena kuongoza kikosi maalum cha kimataifa cha wanamaji kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu ijayo nje ya bahari ya Pembe ya Afrika.
Kikosi hicho kinachoundwa na manowari tisa kutoka nchi tano kinapiga doria eneo la kuanzia Bahari ya Shamu hadi Ghuba ya Aden kuelekea Bahari ya Arabuni na Mlango Bahari wa Hormuz.
Hii ni mara ya nne kwamba Ujerumani imeongoza kikosi maalum cha kijeshi ambacho ni sehemu ya vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi.