BERLIN: Ujerumani kuongeza nguvu sheria za mikutano ya hadhara.
23 Februari 2005Serikali ya Ujerumani inadhamiria kukaza sheria zake ya kukataza mikutano ya hadhara ya wakereketwa ili kupambana na wanasiasa wamrengo wa kulia.
Chama cha Social Demokrat na kile cha kijani vimetishia kwamba mtu yeyote atakayekiuka sheria hizo au kuunga mkono vitendo vya kikatili vya wanazi atakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu gerezani.
Vyama vya Upinzani pia vimeunga mkono pendekezo hilo lakini vikataka kuwepo na mjadala zaidi kuhusiana na suala hilo.Maandamano yaliyopangiwa kufanyika mjini Berlin Mwezi Mei na chama cha mrengo wa kulia NPD umezusha mjadala mkali juu ya kupunguza haki ya kukutana.
Maandamano ya Manazi mamboleo yalifanyika mwezi huu katika sherehe za ukumbusho mjini Dresden,kuadhimisha siku ya shambulio la bomu katika mji huo wakati wa vita vya pili vya dunia.