BERLIN : Ujerumani kumuunga mkono Wolfowitz
22 Machi 2005Matangazo
Ujerumani imeiahidi Marekani kwamba haitozuwiya uteuzi wa Paul Wolfowitz kuwa mkuu mpya wa Benki ya Dunia.
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha N-TV Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amesema amemweleza Rais George W Bush wa Marekani katika mazungumzo ya simu kwamba uteuzi huo hautokwama kwa sababu ya Ujerumani.Ridhaa hiyo ni moja ya ishara kubwa kabisa kuwahi kuonekana kwamba Schroeder anataka kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Ulaya.
Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya leo wanatarajiwa kujadili uteuzi huo tata wa naibu waziri wa ulinzi wa Marekani kushika wadhifa huo.