BERLIN : Ujerumani kufanya uchaguzi na mapema
22 Julai 2005Ujerumani kuwa na uchaguzi mpya baada ya Rais Horst Köhler kulivunja bunge.
Köhler amesema kuptia televisheni ya taifa kwamba amekubaliana na serikali ya Kansela Gerhard Schroeder kuwa haina tena kuungwa mkono inaouhitaji katika kuongoza nchi. Schroeder ameukaribisha uamuzi huo wa kuitisha uchaguzi tarehe 18 mwezi wa Septemba.Amesema atapigania kuchaguliwa tena kutaka kuungwa mkono upya kwa mageuzi yake ya ustawi wa jamii. Shroeder alitaka kufanyika kwa uchaguzi huo na mapema miezi 12 kabla ya muda wake uliopangwa baada ya chama chake cha Social Demokrat SPD kushindwa vibaya katika chaguzi za mikoa mapema mwaka huu.
Chama cha upinzani cha kihafidhina cha Christian Demokrat kinachoongozwa na Angela Merkel hivi sasa kinaongoza kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni.
Mahkama Kuu ya Ujerumani bado inatakiwa kutowa uamuzi iwapo chaguzi huo wa mapema unazingatia katiba au la.