BERLIN: Ujerumani kubana matumizi
16 Oktoba 2005Matangazo
Waziri wa fedha mteule wa Ujerumani bwana Peer Steinbrück amesema Ujerumani inapaswa kuendesha sera ya kubana matumizi ili kurekebisha bajeti .
Bwana Steinbrküc ameeleza katika mahojiano ya gazeti kwamba,ili kuleta utengemavu katika bajeti kuanzia mwaka 2007, Ujerumani lazima upunguze matumizi kiasi cha Euro bilioni 14 na nusu kila mwaka.