BERLIN Ujerumani kubana matumizi:
25 Oktoba 2005Matangazo
Vyama vikuu vya siasa vinavyotarajia kuunda serikali ya mseto hapa nchini, CDU CSU na SD vimetangaza mpango madhubuti wa kubana matumizi.Chini ya mpango huo, Ujerumani inakusudia kupunguza matumizi kiasi cha Euro bilioni 35 hadi kufikia mwaka wa 2007 na hivyo kurejea katika kiwango kisichozidi asilimia tatu katika nakisi.
Hatahivyo hatua za kufikia kwenye lengo hilo bado hazijafahamika, lakini wataalamu wa masuala ya fedha wameeleza wazi kwamba megeuzi katika sera ya kodi hayatasaidia sana wakati huu ambapo mapato ya kodi yamepungua kwa mabilioni ya EURO.