Berlin. Ujerumani ina wasi wasi na wanajeshi wake Afghanistan.
29 Oktoba 2006Matangazo
Kuna wasi wasi nchini Ujerumani kuwa uchapishaji hivi karibuni wa picha zinazoonyesha wanajeshi wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr wakiwa wameshikilia mafuvu ya wafu nchini Afghanistan kunaweza kuathiri maslahi ya kiusalama ya nchi hiyo.
Hii inakuja baada ya maafisa wa wizara ya ulinzi kunukuliwa wakisema kuwa picha hizo zinye kuchukiza zinaweza kuzusha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Bundeswehr nchini Afghanistan na pia zinaweza kuleta matatizo hapa nchini.
Hata hivyo waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble amesema kuwa kwa hivi sasa hakuna sababu ya kuongeza kiwango cha usalama nchini Ujerumani.