BERLIN: Ujerumani haitopeleka vikosi vya kupigana
19 Agosti 2006Matangazo
Ujerumani ipo tayari kuvisaidia vikosi vya Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon,lakini sio kwa vikosi vya ardhi kavu.Baada ya kuwa na kikao maalum cha kamati ya wabunge kuhusu masuala ya kigeni,waziri wa nje Frank-Walter Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari kuwa Ujerumani inaweza kupeleka manowari za kijeshi kusimamia usafirishaji wa silaha nchini Lebanon.Vile vile inaweza kupeleka manowari yenye hospitali na vikosi vya Kijerumani pia vingeweza kusaidia kazi za ugavi na usafirishaji.