BERLIN: Ujerumani haitopeleka majeshi kupigana
18 Agosti 2006Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema, Ujerumani inataka pia kusaidia kijeshi nchini Lebanon,lakini haitopeleka vikosi vya ardhi kavu.Ujerumani ipo tayari kutuma kikosi cha wanamaji kulinda usalama wa njia za baharini nje ya pwani ya Israel na Lebanon.Vile vile inafikiria kupeleka wanajeshi kusaidia kazi za ugavi na usafirishaji aliongezea Kansela Merkel. Kwa mujibu wa Merkel,meli ya kijeshi yenye hospitali inaweza kupelekwa moja kwa moja kutoa matibabu kwa raia waliojeruhiwa.Lakini kushiriki kwa Ujerumani kunategemea maelezo wazi wazi ya dhamana ya vikosi vya kimataifa.Vile vile hatua hiyo itahitaji kuidhinishwa na serikali ya Lebanon na bunge la Ujerumani.