BERLIN : Ujenzi wa uwanja wa ndege Berlin waanza
6 Septemba 2006Matangazo
Kazi ya ujenzi imeanza katika uwanja wa ndege mpya wa kimataifa kwa Berlin.
Meya wa Berlin Klaus Wowereit na Waziri wa Uchukuzi wa Ujerumani Wolfgang Tieefensee walishiriki katika sherehe za uzinduzi katika eneo unakojengwa uwanja huo mashariki mwa mji huo mkuu wa Ujerumani pembezoni mwa uwanja wa Schönefeld.
Uamuzi wa kuendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege huo mpya umekuja baada ya miaka 14 ya mvutano wa kisheria na kisiasa.
Uwanja huo unatazamiwa kufunguliwa hapo mwezi wa Oktoba mwaka 2011 na kuchukuwa nafasi ya viwanja vya ndege vitatu vya Berlin ambavyo vinatumika hivi sasa.