Berlin: Ufumbuzi wa visa vya uhalifu umezidi hapa Ujerumani
9 Juni 2005Matangazo
Polisi ya Ujerumani mwaka jana ilipata ufumbuzi wa idadi kubwa kabisa ya kesi tangu kaunzishwa takwimu za vitendo vya uhalifu nchini. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Otto Schily, amesema karibu visa vyote vya mauaji na mauaji bila ya kukusudia vimetanzuliwa. Alisema sababu moja ni kuweko teknoljia ilio bora, kama vile kufanya majaribio ya viini vya uzazi, kwa njia ya DANN. Waziri huyo alikuwa akizungumzia juu ya kuchapishwa takwimu za karibuni juu ya visa vya uhalifu nchini katika mwaka 2004. Takwimu hizo, hata hivyo, zinaonesha vitendo vya kawaida vya uhalifu vimeongezeka.