Berlin. Time ya washauri wa masuala ya kampeni yazinduliwa.
17 Agosti 2005Matangazo
Mgombea wa kiti cha ukansela nchini Ujerumani wa chama cha upinzani , Angela Merkel , amekitambulisha kikosi chake ambacho anasema ni mahiri cha washauri wa masuala ya kampeni.
Kundi hilo la wanaume sita na wanawake watatu ni pamoja na mtu mmoja mwenye msimamo mkali wa maadili, mtaalamu mwenye msimamo mkali wa masuala ya mabadiliko ya kodi na mama mmoja mwenye watoto saba. Chama cha Merkel cha Christian Democrats kinataka kukiondoa madarakani chama cha kansela wa sasa Gerhard Schröder cha Social democrats katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Septemba 18.