Berlin/Tel Aviv: Serikali kuu ya Ujerumani imelaani shambulio la jana la kusabilia maisha nchini Israel.
26 Desemba 2003Waziri wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer amewatolea mwito Wapalastina na waisrael "wafanye kila liwezekanalo kuzuwia gurudumu la maangamizi,baada ya damu kumwagika mnamo siku kuu ya X-Mas."Matokeo ya mazungumzo ya hivi karibuni kati ya wapalastina na waisrael na juhudi za upatanishi za Misri,yanabidi yahifadhiwe" ameongeza kusema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani aliyetuma pia salam za rambi rambi kwa familia za wahanga na kuwaombea afya njema waaliojeruhiwa.Wimbi la umwagaji damu lililopiga jana mashariki ya kati,limegharimu maisha ya waisrael wanne na mpalastina aliyejiripua huko Tel Aviv.Kabla ya hapo jeshi la wanaanga la israel lilimlenga na kuwauwa viongozi wa wawili wa Jihad huko Gaza-Moqrem Hamid na Nabil Shreihi..Mabomu yaliyoporomoshwa na madege ya kivita ya Israel yaligharimu maisha ya wapalastina wengine wanne,na dazeni kadhaa kujeruhiwa.Moqrem Hamid anatuhumiwa na viongozi wa Israel kuandaa mashambulio kadhaa dhidi ya Israel.Waziri wa ulinzi wa Israel anakutana na viongozi wa kijeshi kusaka njia za kujibu shambulio hilo la jana karibu na Tel Aviv.Jeshi la Israel limeyaazingira maeneo ya utawala wa ndani na nyumba ya mwanaharakati wa kipalastina aliyejiripua jana karibu na Tel Aviv imebomolewa .Djihad wamesema watalipiza kisasi.