BERLIN: Suluhisho la kudumu linategemea uhuru wa wanajeshi wa Kiisraeli
28 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Israel,Tzivi Livni alipokutana na waziri mwenzake wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier mjini Berlin,amesema suluhisho lo lote la kudumu nchini Lebanon linategemea kuachiliwa huru wanajeshi 2 wa Kiisraeli wanaozuiliwa na Hezbollah.Steinmeier, amekataa kuwa Ujerumani inashughulika na suala la kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Hezbollah.Na kuhusu vikosi vya kimataifa vitakavyopelekwa Lebanon,waziri Steinmeier amesema, “Kwa hivi sasa kilicho na umuhimu ni maelezo ya masharti na wajibu utakaotekelezwa huko na wanajeshi wa Ulaya.Hatimae ni suala la idadi yenyewe.”