BERLIN: Suala la Kansela halikupatiwa ufumbuzi
5 Oktoba 2005Matangazo
Duru ya tatu ya mazungumzo kati ya wakuu wa chama cha Social Democrats-SPD cha Kansela Gerhard Schroeder na vyama vya upinzani vya kihafidhina CDU na CSU,kuchunguza uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano imemalizika.Suala kuu la mabishano,nani atakaeiongoza nchi bado halijapatiwa ufumbuzi.Chama cha Social Democrats-SPD kinashikilia kuwa Schroeder abakie kama kansela kwa awamu ya tatu.Lakini chama cha CDU kinasema,Angela Merkel wa CDU ana mamlaka ya kuiongoza serikali mpya kwa sababu vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU kwa pamoja vimeshinda viti 4 zaidi ya chama cha SPD katika uchaguzi wa mwezi Septemba.