BERLIN: Stoiber alaumiwa na wapigaji kura
11 Agosti 2005Matangazo
Huku uchaguzi ukikaribia nchini Ujerumani, wapinzani wanakabiliwa na lawama mpya za kuwatukana wapigaji kura wa eneo la mashariki mwa Ujerumani. Mbunge wa Bavaria, Edmund Stoiber, analaumiwa vikali na wananchi wa mashariki na wengine kutoka eneo lake. Stoiber aliwaelezea wananchi wa mashariki kama watu wasio na matumaini na kutilia shaka uwezo wao wa kupitisha uamuzi juu ya uchaguzi.
Chama chake Stoiber kimetoa taarifa kikisema kwamba Stoiber aliwataja viongozi wa chama kipya cha mrengo wa kushoto kuwa wasio na matumaini yoyote na wala hakuwajumulisha wajerumani wote wa mashariki.