BERLIN: Steinmeier arudi tena Mashariki ya Kati
14 Agosti 2006Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, ataondoka kwenda Mashariki ya Kati kwa ziara yake ya tatu katika kipindi cha mwezi mmoja.
Katika ziara yake Steinmeier analenga kuwahimiza viongozi wa mataifa ya Mashariki ya Kati kusaidia katika juhudi za kutafuta amaniy a kudumu kati ya Israel na kundi la Hezbollah.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Berlin amesema Steinemeier ataanza ziara yake nchini Jordan hii leo na baadaye ataitembelea Syria hapo kesho.
Waziri Steinmeier atakamilisha ziara yake nchini Saudi Arabia kesho kutwa Jumatano na anatarajiwa kuwashawishi viongozi wa mataifa hayo kushiriki kikamilifu kuumaliza mgogoro wa Mashariki ya Kati, hususan Syria, inayosema inawaunga mkono wanamgambo wa Hezbollah.
Israel inailaumu Syria kwa kuwapa silaha wanamgambo wa kundi la Hezbollah.