BERLIN: Siniora ameshukuru msaada wa Ujerumani
28 Septemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora akiwa ziarani mjini Berlin ametoa shukrani zake kwa Kansela Angela Merkel na bunge la Ujerumani kwa msaada unaotolewa kwa Lebanon.Baada ya mkutano wao,Kansela Merkel alisema,Ujerumani itatoa mchango wake kutafuta suluhisho la kisiasa katika mgogoro wa Lebanon na Israel.Madola jirani pia lazima yasadikishwe kuwa njia iliyopo ni kuwa na suluhisho la kisiasa tu,aliongezea Merkel.