BERLIN : Shule ya Kiislam yakabiliwa na hatua ya kufungwa
7 Agosti 2005Matangazo
Serikali imekatisha michango kwa shule moja ya Kiislam kusini mwa Ujerumani na kuamuwa kutoongeza muda wa leseni yake kwa sababu ya kushukiwa kuwa na uhusiano wa karibu na kundi moja la Kiislam la itikadi kali.
Shule hiyo ya Kiislam ya Munich inakabiliwa na hatua ya kufungwa kwa sababu idara za ujasusi zinaona shirika linaloiendesha shule hiyo lina uhusiano wa karibu na tawi la Muslim Brotherhood lilioko Ujerumani.
Shule hiyo imetowa taarifa ikiaahidi kuchukuwa hatua ya kisheria dhidi ya uamuzi huo na kulalamika kwamba Waislamu wamekuwa wakionewa kwa kufanywa wahanga katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa tarehe 18 mwezi wa Septemba.