BERLIN: Shaka kuhusu uchaguzi wa Iran
26 Juni 2005Matangazo
Ujerumani imeeleza wasiwasi wake kuhusu uchaguzi wa rais uliofanywa hivi karibuni nchini Iran.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer amesema uchaguzi huo umeonyesha dosari fulani.Vile vile ametoa mwito kwa Iran ihakikishe kuwa,mradi wake wa kinuklia ni kwa matumizi ya amani tu kama inavyodaiwa na serikali ya nchi hiyo.Fischer amesema, Ujerumani,Uingereza na Ufaransa zitaendelea kujadiliana na Iran kuhusu mradi wake wa kinuklia,hata baada ya kuchaguliwa kwa meya wa kihafidhin wa Teheran,Mahmoud Ahmadinejad.Msemaji wa serikali ya Marekani pia ameeleza wasiwasi wa Washington kuhusu uchaguzi wa Iran,akitaja udanganyifu wa uchaguzi na hatua ya kupiga marufuku zaidi ya watu 1,000 waliotaka kugombea uchaguzi.