Berlin. Serikali ya Ujerumani yawarejesha raia wake waliokwama Uturuki
14 Mei 2005Matangazo
.
Serikali ya Ujerumani imeingilia kati na kuwarejesha nyumbani maelfu ya raia wake waliokwama nchini Uturuki. Watalii hao wamekwama baada ya wachunguzi wa masuala ya usalama wa ndege kulipiga marufuku shirika la ndege la Uturuki Onur Air kutua katika viwanja vya ndege nchini Ujerumani, Uswisi, Uholanzi na Ufaransa. Ujerumani imesema kuwa inataka uhakikisho kutoka Uturuki kuwa ndege mbadala zitaruhusiwa kutua.
Msemaji wa shirika la ndege la Onur amekana madai hayo kwamba ndege 28 za shirika hilo si salama na kusema kuwa shirika hilo linapanga kuchukua hatua za kisheria.